Aliyekuwa Mkuu wa Shirika la upepelezi nchini Marekani FBI James Comey
Aliyekuwa
Mkuu wa Shirika la upelelezi la FBI nchini Marekani James Comey
ameanza kutoa ushahidi mbele ya Maseneta nchini Marekani kuhusu madai ya
Urusi kuingilia Uchaguzi Mkuu wa Marekani mwaka uliopita.
Comey
ambaye aliyefutwa kazi na Trump baada ya kuingia Ofisini, ameishtumu
Ikulu ya Marekani kwa kumharibia jina na kusema uongo kuhusu Shirika
hilo.
Mkuu huyo wa zamani wa FBI amewaambia Maseneta waliomhoji kuwa alikuwa na mazungmzo ya siri na rais Trump.
Aidha, ameshtumu matamshi ya Ikulu ya Marekani kuwa, FBI imekosa imani naye.
Trump alimfuta kazi Comey tarehe 9 mwezi Mei, baada ya FBI kutangaza kuchunguza madai ya Urusi kuingilia Uchaguzi wa Marekani, madai ambayo Urusi imekanusha.
Comey amesema, Trump alimwambia asitishe zoezi la FBI kumchunguza Michael Flynn, aliyekuwa mshauri wake wa maswala ya usalama kwa madai kuwa alikuwa na mawasiliano ya karibu na maafisa wa Urusi kipindi cha Uchaguzi.
Wachambuzi wa siasa wanasema kuwa, kuna uwezekano wa ripoti ya Maseneta hao ikaathiri uongozi wa rais Trump.

0 maoni:
Post a Comment