Fahamu Jinsi Ya Kufanikiwa: Sehemu ya Kwanza


Kumekuwa na tafsiri nyingi sana kuhusu mafanikio katika maisha ya mtu ;
  • wengine wametafrsiri mafanikio kama kufikia malengo fulani uliojiwekea,
  • wengine wamesema mafanikio ni uwezo wa kujikimu au kupata mahitaji ya muhimu kama vile chakula mavazi malazi ,
  • wengine wameamini mafanikio ni kusoma sana na kufikia ngazi ya juu kielimu,
  • wapo wanaotafsiri mafanikio ni kuwa na mali nyingi nyumba za kifahari, magari ya thamani na pesa nying,
  • wengine wametafsiri mafanikio kama uwezo wa mtu kuuridhisha moyo wake na kupata matamanio ya nafsi yake,
  • wengine wanaamini mafanikio ni kuwa mtu maarufu(kujulikana) ama kuwa na nafasi fulani inayoheshimika katika jami,
Jambo la hatari zaidi ni pale mtu anapo pambana kutafuta mafanikio pasipo kujua tafsiri sahihi ya mafanikio au  nini maana ya kufanikiwa katika maisha
Kutokujua maana sahihi ya mafanikio kumefanya watu wasifahamu njia sahihi ya kuyapata hayo mafanikio kwa sababu ni vigumu sana kutafuta kitu usichokijua kikoje na kina muonekano  gani kwa sababu ikitokea umekipata kitu hicho hautajua kama umekipata kwa sababu haujui njia utakazo tumia kukipata kitu hicho itakuwa ni kubahatisha utafanya kila utakachoambiwa ufanye ili ukipate kitu hicho ni kama mtu anayekwenda kituo cha mabasi ili asafiri angali hajui anapokwenda mtu huyu huweza kupanda gari lolote pasipokujali kuwa amepanda gari sahihi ama sio sahihi pia huweza kushukia kituo chochote kile maadamu ameona watu wanashuka kwa sababu hajui anapokwenda.
Tafsiri nyingi zisizo sahihi kuhusu mafanikio kumewafanya watu wengi kuishi maisha ya kubahatisha na wengine wamejikuta wakitumia njia zisizo sahihi  katika kutafuta kile wanachoamini kuwa ni mafanikio.
Kila mtu anatamani afanikiwe katika maisha yake  Je una tafsiri gani ya mafanikio katika maisha yako je unaamini kitu gani kitakufanya ufanikiwe kwenye maisha je Mungu aliumba wengine wafanikiwe na wengine wasifanikiwe katika maisha? Je mafanikio huja kwa bahati ama yanatafutwa? Majibu yote haya tutayapata kwenye mfululizo wa somo hili linaloenda kwa jina la FANIKIWA katika somo hili tutajifunza kanuni muhimu na mambo yote ya msingi yanayomfanya mtu afanikiwe katika maisha. Itaendelea………………………
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment