Jengo liliporomoka katika mtaa wa Kware, jimboni Embakasi jijini NairobiKenyaRedCross
Watu
wanne ambao ni mama na watoto wake watatu hawajapatikana baada ya jengo
la orofa saba kuporomoka Mashariki mwa jiji kuu la Kenya, Nairobi
Jumatatu usiku.
Shirika la Msalaba mwekundu nchini humo limesema tayari mamia ya watu waliokuwa wanaishi katika jengo hilo wameokolewa.
Msemaji wa kitengo maalum cha uokozi Pius Masai, ameeleza kuwa kufikia mchana, wapangaji 128 walikuwa wameokolewa na kutambuliwa.
Hata hivyo, bado kuna wasiwasi kuwa huenda kuwa idadi zaidi ya watu ambao wamefukiwa na vifusi vya jengo hilo lililopo katika mtaa wa Kware katika jimbo la Embakasi.
Polisi wanasema wakaazi wa jengo walikuwa wameonywa mapema kuhama baada ya nyufa katika kuta za orofa hilo kuanza kuonekana.
Musundi, mmoja wa wakaazi wa mtaa huo ameliambia Shirika la Habari la Ufaransa la AFP kuwa, kuanguka kwa jengo hilo ni jambo ambalo lilitarajiwa.
Hii sio mara ya kwanza kwa jengo la kupanga kuanguka jijini Nairobi na kusababisha madhara makubwa ikiwa ni pamoja na vifo na majeraha.
Wataalam wa ujenzi wamebaini kuwa wamiliki wengi wa majengo ya kupanga katika jiji hilo, hawazingatii sheria za ujenzi.

0 maoni:
Post a Comment