Majimbo mawili ya Marekani yatoa malalamiko dhidi ya Trump



mediaMalalamiko haya yanasema kuwa rais wa Marekani anakiuka sheria dhidi ya rushwa kwa sababu hakukata mahusiano na makampuni yake yanayosimamiwa rasmi na wanae wa kiume tangu uchaguzi.Reuters
Mawaziri wa Sheria wa Maryland na Wilaya ya Columbia waliwasilisha malalamiko yao Jumatatu Juni 12 dhidi ya rais wa Marekani Donald Trump. Malalamiko hayo yanaeleza kwamba rais wa Marekani anakiuka sheria dhidi ya rushwa kwa sababu hakukata mahusiano na makamuni yake yanayosimamiwa rasmi na wanae wa kiume tangu uchaguzi.
Nakala hiyo inasema kuwa sera ya Donald Trump iko chini ya ushawishi wa nchi za nje ambazo zinafanya biashara na makampuni ya bilionea huyo.
Kwa mujibu wa mwandishi wa RFI mjini Washington, Anne-Marie Capomaccio, haya ni malalamiko ya kwanza ya aina hii. Majimbo mawili ya Marekani yakitoa malalamiko dhidi ya rais wa Marekani kwa ukiukwaji wa sheria za rushwa. Lengo la mpango huo, mawaziri wawili wa Sheria wanataka kufanyike ukaguzi wa shughuli za Donald Trump, na wakati huo huo, kutoa taarifa ya mapato ya kodi ambayo kamwe hayajatangazwa kwa umma, tofauti na mila ya tangu miaka ya 1970.
Hayo yakijiri amri ya Donald Trump kuzuia raia kutoka nchi za kiislamu imepata pigo jingine mahakamani
Mahakama ya rufaa nchini Marekani imemua kuwa uamuzi wa kuzuia mpango uliofanyiwa marekebisho wa marufuku ya rais Donald Trump kuzuia watu kutoka nchi sita za kiislamu utaendelea kuwepo. Majaji wamesema kuwa amri hiyo inakiuka sheria zilizopo za uhamiaji.
Rufaa hiyo iliyowasilishwa katika mahakama ya rufaa ya San Fransisco, ni kufuatia uamuzi uliotolewa kupinga raia wengi wao wakiwa kutoka nchi za Kiislam kuingia Marekani.
Hata hivyo mahakama haikusema kuwa serikali inatakiwa kuzipitia upya taratibu za ukaguzi kwa watu wanaoingia nchini humo.
Msemaji wa Ikulu ya Marekani Sean Spicer ameutetea msimamo huo wa rais Trump, akisema amri hiyo ilitolewa kwa ajili ya ulinzi wa Marekani.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment