Mkongwe wa muziki wa taarab,
Bi. Khadija Omar Kopa amedai muziki wa wao unaonekana kama umepoteza
ladha kwa sababu ya nyimbo zao kupigwa sana sehemu ya kuuza vilevi na
kupotezewa katika vyombo vya habari.
Khadija
amezungumza hayo akiwa kwenye uzinduzi wa video ya Saida Karoli
'Orugambo na kusema kwamba muziki wa taarabu umeshushwa na watu wachache
walioruhusu nyimbo zao kuchezwa 'bar' kitu kinachopelekea hata wapenzi
wa muziki kususia matamasha yao yakiandaliwa.
"Muziki wetu umekosa thamani
baada ya kuanza kupigwa kwenye ma- bar, unakuta nyimbo zinapigwa bar
muda wote mtu ananua maji yake ya 1500 anasikiliza nyimbo anarudi
nyumbani, saa ngapi atakuja kwenye show wakati bar anapata bure, lakini
watu wa media nao wametupotezea sana kiasi kwamba wamefanya taarabu ni
ya kipindi maalumu siyo kama bongo fleva au hip hop wao nyimbo zao
zinapigwa kila muda, Wao ndio waliotufanya tujulikane lakini pia wao
ndiyo wanatupoteza", Khadija alisema.
Akizungumzia ujio wa Saida Karoli tena
kwenye 'game' Khadija amesema sanaa ilimkosa mtu mwenye ladha ya asili
kwa muda mrefu na ujio wake ni burudani kwa wasanii na wapenda muziki
mzuri.
"Tulim-miss sana Saida sema
wasanii tunajijua matatizo yetu, Uongozi ukiwa mbovu utakufanya upotee
lakini ni vizuri amerudi tena na sisi tunamkaribisha, hapa tayari
nimeshaweka mazingira ya kuweza kufanya kolabo. Naomba tumpe ushirikiano
ule tuliokuwa tunamuonyesha zamani maana kipaji na uwezo wake
unajionesha", Khadija aliongeza.
0 maoni:
Post a Comment