Wanajeshi wa jeshi la DRC wakijiandaa kuingia kwenye uwanja wa mapambanoReuters
Mwanajeshi
mmoja na wanamgambo 12 wameuawa katika makabiliano yaliyotokea siku ya
jumamosi katika jimbo lenye kushuhudia utovu wa usalama Kivu ya
kaskazini nchini DRC.
Msemaji wa
jeshi la DRC luteni Jules Tshikudi amethibitisha wapiganaji 12 wa
Maiamai na afisa wa jeshi la DRC kuuawa katika makabiliano jana jumamosi
katika kuwania eneo la Kibasha.Kundi la Maimai limekuwa likiendesha uasi katika eneo hilo ambapo katika vita ya Congo kati ya mwaka 1998 na 2003 makundi kadhaa yanayomiliki silaha yaliibuka kupambana dhidi ya vikosi vya Uganda au Rwanda lakini baadhi ya makundi hayo hayakusalimisha silaha tangu wakati huo.
Makabiliano ya jumamosi yalizuka baada ya wapiganaji wa Maimai kuvamia na kushambulia kituo cha kijeshi katika eneo la Kibasha ambalo bado linadhibitiwa na serikali na kushuhudia wakazi wakikimbia.
Eneo la Kabasha lipo umbali wa kilomita 24 kusini mwa mji wa Beni, mji ulioshuhudia wimbi a vurugu tangu mwaka 2014 huku takribani 700 wakiuawa wengi wao kuchinjwa hadi kufa
0 maoni:
Post a Comment