Z Anto sio wa spoti spoti, adai anamiliki fremu 70 za biashara






Msanii wa muziki, Z Anto amefunguka kwa kudai kuwa yeye ni mfanyabisha mkubwa ambaye anamiliki zaidi ya fremu 70 za biashara.

Z AntoMuimbaji huyo ameiambia Bongo5 kuwa kwa muda mrefu amekuwa akijihusisha na biashara tofauti tofauti akiwa nje ya muziki.
“Mara nyingi wasanii wana maneno mengi pasipo vitendo, ningekuwa karibu katika mazingira yangu ya biashara ningekwambia angalia aina ya biashara ambayo nafanya. Mimi ni mmliki wa fremu za biashara kama 70 na kitu hivi,” alisema Z Anto.
Aiongeza, “Lakini pamoja na hilo pia na biashara nyingine ambazo nafanya na kila siku naendelea kutafuta biashara mpya za kufanya,”
Katika hatua nyingine muimbaji huyo amedai kwa sasa anajipanga kuitambulisha kampuni yake mpya itayokuwa inasimamiwa muziki wake.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment