Wakiristo duniani wajiandaa kusherehekea Sikukuu ya Krismasi


mediaMji wa Bethlehem ulivyopambwa kusherehekea sikukuu ya Krismasiyoutube
Shamrashamra za Krismasi zimeanza kote duniani, kueleka siku ya Jumatatu, siku ambayo Wakiristo wataadhimisha sikukuu ya kuzaliwa kwa Mwokozi Yesu Kristo.
Wakiristo wanaamini kuwa kuzaliwa kwa Yesu Kristo kuliwaletea ukombozi.
Tarehe 25 mwezi Desemba kila mwaka, Wakiristo kote duniani hutumia siku hiyo kwenda Makanisani na baadaye kusherehekea pamoja  nyumbani na maeneo mengine kwa kula vyakula na kutoa zawadi.
Mjini Bethlehem nchini Israel, mji ambao Wakiristo wanaamini kuwa Yesu alizaliwa, mwaka huu shamrashamra zinashuhudiwa  lakini sio kwa kiasi kikubwa.
Wasiwasi unashuhudiwa na watalii wengi, hawajakwenda katika mji huo kwa kuhofia usalama wao.
Hatua hii inakuja baada ya Marekani hivi karibuni, kutambua mji wa Jerusalem kama makao makuu ya Israel hatua ambayo imeikasirisha Palestina na mataifa ya Kiislamu na yale ya kiarabu.
Wiki hii, kulikuwa na mkutano wa dharura wa Umoja wa Mataifa kulaani hatua hiyo ya Marekani.
Kumeendelea kushuhudiwa makabiliano kati ya waandamanaji wa Kipalestina na wanajeshi wa Israel na kufikia siku ya Jumapili, rais wa Palestina 12 wamepoteza maisha.
Uamuzi wa Marekani, umeelezwa na washirika wa Palestina kuwa, umehatarisha uwezekano wa kupatikana kwa amani kati yake na Israel.
Sikukuu njema ya Krismasi.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment