Mshambulio kali la
Roberto Firmino liliisaidia Liverpool kutoka nyuma na kupata sare katika
mechi ya ligi ya Uingereza ambayo Arsenal ilifunga mabao matatu katika
dakika tano za kipindi cha pili.
Arsenal walikuwa nyuma 2-0 baada
ya Phillipe Coutinho kufunga kwa kichwa naye Mohammed Salah akaongeza
bao la pili katika kipindi cha pili.Lakini Arsenal iliimarika huku Alexis Sanchez akifunga kwa kichwa kufuatia krosi muruwa iliopigwa na beki wa kulia wa Arsenal Hector Bellerin kabla ya Granit Zhaka kufunga kombora la mbali ambalo lilimshinda kipa wa Liverpool Simon Mignolet.
Dakika mbili baadaye Mesut Ozil aliiweka kifua mbele Arsenal baada ya kufunga bao zuri kufuatia gusa ni guse na mshambuliaji wa Arsenal Lacazette.
- Liverpool 'yainyoa' Arsenal
- Liverpool yaichapa kichapo kizito Arsenal
- Mchezaji wa Nigeria aihama klabu ya Arsenal
Lakini ilikuwa Liverpool iliosawazisha baada ya Firmino kuwachwa pekee katika safu ya Arsenal na kumfunga kipa Cech ambaye alishindwa kuupangua mpira huo na badala yake akaupungua na kuingia katika wavu wa goli lake.
Matokeo hayo yanaonyesha kuwa Liverpool imehifadhi nafasi yake katika jedwali la ligi huku nayo Arsenal ikisalia katika nafasi ya tano ikiwa nyuma ya Liverpool kwa pointi moja.
0 maoni:
Post a Comment