Barcelona
ilionyesha mchezo mzuri ugenini na kupata ushindi dhidi ya Real Madrid
ambayo imeondolewa katika kuwania taji la ligi ya Uhispania.
Shambulio
la kipindi cha pili la Luis Suarez na penalti ya Lionel Messi baada ya
Dani Carvajal kupewa kadi nyekundu kwa kunawa mpira, bao lililosaidia
Barcelona kupanda juu ya jedwali kwa alama 14 dhidi ya Real.Karim Benzema alipiga mwamba wa goli na kukosa nafasi mbili za wazi katika kipindi cha kwanza , lakini timu hiyo ya nyumbani ilibaki bila jibu katika mechi hiyo ya El Clasico.
Los Blancos ilianza huku Gareth Bale akiwa benchi, na ijapokuwa alimlazimu kipa Marc-Andre ter Stegen kuokoa mipira baada ya kuingizwa kufuatia kutolewa kwa Carvajal, mshambuliaji huyo wa Wales alishindwa kuokoa timu yake.
- Barca yaichapa Madrid El Clasico
- Barcelona kutoana jasho na Real Madrid katika 'El Clasico'
- Debi ya Manchester kuchezewa Marekani
Ni mara ya kwanza Barcelona imeweza kushinda mechi tatu za ugenini mfululizo katika uwanja wa Bernabeu, na matokeo hayo yanakiwacha kikosi cha Zinedine Zidane katika nafasi ya nne.
0 maoni:
Post a Comment