Jeshi
la Polisi katika Mkoa wa Kipolisi Tarime/Rorya mkoani Mara limemkamata
na kumfikisha mahakamani Mwalimu wa Shule ya Msingi Itiryo kwa tuhuma za
kuwabaka wanafunzi 9 wa darasa la kwanza.
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Henry
Mwaibambe, alithibitisha kuwa wamemkamata Mwalimu Swamwel Daniel ambaye
anatuhumiwa kuwabaka wanafunzi wa darasa la kwanza wenye umri kati ya
miaka 7 hadi 9.
Kamanda
Mwaibambe alisema kuwa mwalimu huyo anadaiwa kutenda kitendo hicho kwa
nyakati tofauti kati ya tarehe 30 Novemba hadi tarehe 6 Disemba. Aidha
amesema walimkamata mtuhumiwa huyo alipokuwa akijiandaa kutoka nje ya
nchi.
Mwalimu
hiyo alifikishwa mahakamani Disemba 12 mwaka huu na kufunguliwa kesi ya
jinai namba 682 ambayo inatarajiwa kutajwa Disemba 28 mwaka huu.
Aidha,
Mwaibambe alisema kuwa ushahidi na vitu vyote vinavyotakiwa katika kesi
hiyo vimekamilika na hivyo ameiomba mahakama kama itawezekana kesi hiyo
isikilizwe ndani ya muda mfupi.
A
0 maoni:
Post a Comment