\
Mwanamke
mmoja ajulikanaye kama Sandhya Rani mwenye umri wa miaka 25 huko Kusini
mwa nchini India ameuawa kwa kuchomwa moto na mpenzi wake baada ya
kukataa kuchumbiwa naye.
Kwa
mujibu wa Jeshi la Polisi katika jimbo hilo, mashuhuda wa tukio hilo
wanasema waliona mwanaume huyo akifuata mwanamke huyo na wakaanza
kuzungumza kwa kubishana na ndipo mwanaume huyo alipochukua mafuta ya
taa aliyokuwa ametembea nayo na kummwagia binti huyo kisha kumuwasha
moto.
Inaelezwa kuwa watu walijaribu kumwokoa binti huyo lakini alikuwa ameungua sana na alifariki akiwa njiani akipelekwa hospitali.
Inaelezwa
pia kuwa wawili hao wamewahi kufanya kazi ofisi moja. Polisi jimboni
humo tayari wamemkamata mwanaume huyo aliyetambulishwa kwa jina la
Karthika Vanga.
0 maoni:
Post a Comment