Shirika la ndege la QatarReuters
Mauritania
na Gabon yameungana na Libya na Misri kutoka barani Afrika, kuunga
mkono hatua ya Qatar kutengwa na mataifa ya kiarabu kwa madai ya kuunga
mkono makundi ya kigaidi.
Wizara
ya Mambo ya nje ya Mauritania amesema sera za Qatar zinaunga mkono wazi
makundi ya kijihadi ambazo zimesababisha vifo vya maelfu ya watu
duniani.'Sera za Qatar zinaunga mkono makundi ya kigaidi,” Imesema taarifa kutoka Wizara ya Mambo ya nje.
Gabon ambayo inafahamika kwa uzalishaji wa mafuta barani Afrika, imeishtumu Qatar imeshindwa kuheshimu sheria za Kimataifa kupambana na ugaidi.
Aidha, Wizara ya Mambo ya nje ya nchi hiyo imesema Qatar kwa muda mrefu imeendelea kuyaunga mkono makundi ya waasi.
Wakati uo huo, rais wa Marekani Donald Trump ameyataka mataifa ya Ghuba kuungana katika vita dhidi ya ugaidi na itikadi kali, baada ya kuusifu msimamo wa Saudi Arabia.
Trump ametoa kauli hii baada ya kumpigia simu Mfalme Salman wa Saudi Arabia na kumhakikishia kuwa anaunga mkono hatua ambayo ilichukuliwa na mataifa kadhaa ya kiarabu kusitisha ushirikiano wa kidiplomasia na Qatar kwa mada kuwa inaunga mkono makundi ya kigaidi.
Qatar imekanusha madai hayo na kusema hakuna ushahidi kuonesha kuwa inaunga mkono ugaidi.
Saudi Arabia imesitisha safari za ndege kati ya nchi hizo mbili huku Bahrain ikitaka raia wa Qatar kuondoka nchini humo kwa muda wa siku 14.
0 maoni:
Post a Comment