Mtu mmoja (75) amefariki
katika ajali ya moto huku wengine wawili wakiwa wamejeruhiwa vibaya
(wote wa familia moja) huko Lumumba Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza
siku ya Ijumaa, ambapo mpaka sasa chanzo cha moto huo bado
hakijajulikana.
Tukio
hilo limetokea ya majira 12:30 jioni mtaa wa Lumumba ambapo inadaiwa
kwamba kabla ya ajali hiyo kutokea marehemu alikua ndani ya nyumba
yake pamoja na watoto wake, ndipo ghafla ulizuka moto mkali uliokuwa
unaunguza nyumba yake, na kwamba kutokana na taharuki marehemu alianza
kukusanya mali zake ndani ili aweze kutoka nazo nje ndipo kwa bahati
mbaya moto ulimzidia na yeye kushindwa kutoka nje na kupelekea kuungua
zaidi na baadae kufariki dunia.
Hata hivyo inasemekana kwamba kutokana
na miundombinu mibovu ndiyo iliyopelekea kukosa haraka msaada wa
zimamoto ambapo ukuta uliopo jirani na maeneo hayo ulipelekea gari la
wanajeshi wa zimamoto pamoja na jeshi la polisi kufika eneo la tukio kwa
kuchelewa na kushindwa kuokoa maisha ya mfanyabiashara Maduhu Masunga,
ingawa waliweza kudhibiti moto usiharibu maeneo mengine ya jirani.
Kamanda wa polisi mkoa wa mwanza Ahmed
Msangi anatoa pole kwa wanafamilia wa marehemu, ndugu, jamaa na marafiki
kwa msiba akini pia anawaombea majeruhi wapone haraka na kuwataka
wanafamilia waendele kuwa wavumilivu katika kipindi hiki ambapo mwili wa
marehemu bado unafanyiwa uchunguzi, na kuwaasa wananchi kujitahidi
kuweka vizuri miundombinu ya umeme.
Aidha thamani ya mali na vitu
vilivyoteketea katika ajali hiyo ya moto bado haijafahamika, jeshi la
polisi pamoja na jeshi la zima moto kwa kushirikiana na tanesco
wanaendelea kufanya uchunguzi na upelelezi kuhusiana na tukio hilo ili
kujua chanzo cha moto huo, majeruhi Ngalula Maduhu 39, Brian Maduhu 26,
wamepelekwa hospitali ya mkoa ya Sekou Toure kwa ajili ya matibabu na
hali zao zinaendelea viz
0 maoni:
Post a Comment