PICHA 7: Nyumba 3 zinazotajwa kuwa za ajabu zinaoelea kwenye maji



Kila siku duniani kunafunguliwa Hoteli, sehemu za starehe na sehemu za mapumziko zenye upekee kulingana na mazingira na namna ya kuvutia watu ili kukuza biashara.
Leo June 18, 2017 nimekusogezea nyumba tatu zinazoelea kwenye maji ambazo ni maalumu kwa ajili ya mapumziko.
Floating Summer House
Nyumba hii ina ghorofa mbili ambayo inapatikana Canada kwenye Ziwa Huron. Nyumba hii hutumika kama makazi ya majira ya joto kwa wapenzi wenye asili ya Cincinnati. Ilimalika ujenzi wake mwaka 2008 ikiwa ni moja ya projects za mwanzo za MOS Architects



Belgrade apartments
Hizi ni hostel na apartments ambazo zinaitwa ArkaBarka zipo katika ukingo wa Mto Danube, Belgrade. Katika jengo hili ambalo huelea kwenye maji lina mambo mengi ya anasa vikiwemo sauna na bar. Zimejengwa kwa kiwango cha hali ya juu ambapo vyumba vyake vinaanzia euro 25.50 na bei zote hujumuisha breakfast na WiFi.


Maldives floating house
Maldives Floating House ilibuniwa na msanifu wa majengo wa Singapore anayeitwa Dymitr Malcew. Kwa mujibu wake ni kuwa alitaka kutengeneza kitu ambacho kitawaruhusu watu kuukubali uhuru na asili. Nyumba ina vyumba viwili vya kulala, vyoo viwili, chumba cha kupumzika na jiko. Nyumba hii ina uwezo wa kusogea kutoka sehemu moja hadi nyingine.


UTAJIRI WA BAKHRESA: Hoteli ya kisasa anayojenga baharini Zanzibar
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment