Mapema leo kulikuwa na taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu Mtangazaji wa Azam TV Fatna Ramole
kutojulikana mahali alipo kwa zaidi ya saa 48 na zikatolewa taarifa
nyingine leo mchana kuwa amepatikana akiwa Hospitali baada ya kupata
ajali maeneo ya Chuo cha Ustawi, Bamaga.
Baada ya taarifa za kupatikana kwake jichopembuzi
imempata dada yake anayeitwa Lulu Ramole ili kujua kilichotokea naye kathibitisha kuwa amepatikana ingawa hakuwa na uwezo kuzungumza zaidi akisema taarifa zaidi ziko Polisi.
>>“Nipo hapa Polisi tunamalizia. Tumeweza kumfuata asanteni tumempata. Siwezi kuongea chochote cha zaidi taarifa zipo Polisi.” – Lulu Ramole.

0 maoni:
Post a Comment