Kilele 77

Kilele 77



VIWANGO vya viingilio katika Maonesho ya Kimataifa ya Kibiashara katika kilele chake ambako ni kesho, vimeongezeka kwaajili ya siku hiyo.
Mamlaka ya maendeleo ya biashara (Tantrade) ambapo mkubwa badala ya kulipa Sh 3000 atalipa Sh 4000 huku watoto wakilipa Sh 1000 ile ya siku zote.
Akiizungumzia siku hiyo Mkuu Wa kitengo cha Mawasiliano wa Tantrade, Theresia Chilambo alisema pamoja na mabadiliko hayo ya viingilio wananchi wafike katika viwanja vya sabasaba kuona teknolojia na bidhaa mpya ambazo zimeletwa katika amaonesho hayo.
Katika maonesho haya kuna faida ya nyingi manunuzi, kujifunza na kutalii, hivyo fursa hizo ni muhimu kwa watoto na watu wazima pia ndiyo maana huwa tunaliangalia suala hilo kwa jicho la kipekee tunapopanga kiingilio.
"Kuna utaratibu mzuri ambao hautamchosha mtu akija pia usalama utakuepo, watu watapata fursa mbalimbali za biashara andani na za nje ya nchi," alisema Theresia.
Alisema lengo la kuweka kiingilio hicho ni kuhakikisha Mwananchi wote wanapata nafasi ya kuingia kwenye maonesho hayo huku wakiwapa watoto upendeleo wa kiingilio kidogo ili kuwajengea.
Maonesho hayo yalifunguliwa Julai mosi na Rais John Magufuli na yataendelea kwa siku tano zaidi badala ya Rais kuomba siku ziongezwe.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment