Mkongwe wa muziki wa bongo fleva
Rehema Chalamila 'Ray C' amedai kumfunga mwizi aliyedukua (hack) ukurasa
wake wa Instagram uliokuwa na wafuasi zaidi ya laki tano na kusema
kwamba hataweza kuvumilia wezi kuendelea kuwepo mitaani.
Ray
C amefunguka hayo siku chache zilizopita alipokuwepo kwenye Heshima ya
Bongo fleva kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa kupitia East
Africa radio huku akiesema, wezi hao wa mtandaoni wanarudisha wasanii
nyuma katika kufanya shughuli zao.
"Mwizi aliyedukua
(hack) akaunti yangu amenirudisha sana nyuma kwani nimeshindwa kufanya
matangazo ya video ya wimbo wangu, matokeo yake nimetumia nguvu kubwa
sana nilipouachia. Nikimkamata huyo mtu aliyenifanyia hivyo cha kwanza
nitamnasa kofi kwa kunipa kazi cha pili lazima nimfikishe polisi na
mwisho wake ni Segerea. Siwezi kuendelea kuvumilia watuibie halafu
waendelee kukaa mitaani kwani watatutesa sana," Ray C.
Pamoja na hayo Ray C ameongeza kwamba "Mimi
akaunti yangu haijapotea kabisa kwani naiona ikiweka matangazo
mbalimbali yaani nikimkamata sitamwambia anipe asilimia kumi bali atatoa
pesa yote kwani nitahesababu tangazo la kwanza mpaka la mwisho ili
kujua ni kiasi gani cha pesa anatakiwa anipe maana wameshazoea," aliongeza
0 maoni:
Post a Comment