Kampuni ya Sportpesa nchini umesema
muda wowote kutokea sasa ugeni wa kwanza kutoka timu ya Everton
utawasili kwa kuwa maandalizi yote yamekamilika.
Mkurugenzi wa Utawala wa SportPesa, Abbas Tarimba.
Hayo
yamebainishwa na Mkurugenzi wa Utawala wa SportPesa, Abbas Tarimba kwa
kusema ujio wa Everton hivi sasa ni uhakika bila ya kuwa na shaka yeyote
huku akidai kiungo na nahodha wa zamani wa timu hiyo, Leon Osman kuwa
anatarajiwa kuanza kufika Julai 8 kabla ya kikosi chote kitakachominyana
na Gor Mahia ya kutokea Kenya.
Mbali na hilo, Tarimba amewaambia wadau
wa soka kuwa siku hiyo kutakuwa na kila aina ya burudani kutoka kwa
magwiji hao tofauti na mpira wa uwanjani dakika 90.
Kiungo na nahodha wa zamani wa Everton, Leon Osman.
"Kuna vitu vingi vitafanyika
baada ya mchezo huo kwa maana Everton watazunguka na baiskeli Jijini
Dar es Salaam ili kuweza kuutukuza na kuutangaza utalii wa Tanzania
lakini vile vile Julai 8 na 9 Leon Osman atachukuliwa na Bodi ya Utalii
kupelekwa hifadhi ya Ngorongoro. Kwa kweli mambo ni makubwa sana
yatakayo kuwepo kwa siku hiyo", amesema Tarimba.
Pamoja na hayo, Tarimba amesema tiketi
za kuweza kuhudhuria mtanange huo ambapo bei ya chini imepangwa kuwa
shilingi elfu 3 huku VIP ikiwa ni shilingi elfu 8.
"Kuna tiketi elfu
8 zitakazotolewa bure kwa wachezaji wetu wa 'Sport Betting' kwa upande
huu wa Sportpesa pamoja na watakao kwenda kuangalia mpira huku wakiwa
wamevaa na jezi za Sportpesa, miongoni mwao watapata tiketi hizi za
mualiko wa bure na watakaa VIP. Ni kitu kikubwa ambacho kitafanya
watanzania walio wengi kuhudhuria mechi hii”, amesisitiza Tarimba.
0 maoni:
Post a Comment