Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akizungumza na vyombo vya habari mjini Dodoma juzi, alisema ubadilishaji wa hati za kumiliki viwanja na maeneo hayo kwa miaka 99 unatolewa bure bila kutozwa gharama zozote na utaanza Julai 10, mwaka huu ambako orodha ya wananchi watakaonza kupata itatolewa.
Lukuvi alisema wizara itatoa orodha ya wananchi wa kwanza wa kupata hati hizo mpya na wananchi hao watapitia manispaa ili kuhakiki nyaraka zao na ndipo watafika kwa kamishna wa ardhi ili kupewa hati hizo mpya.
“Wananchi kabla ya kwenda wizarani kwenye kwenye ofisi za Kanda mjini Dodoma, inatakiwa kupitia manispaa na kuhakiki taarifa zao na kama wanadaiwa walipe madeni yao hadi mwaka huu 2017/18,” alisema Lukuvi.
Katika kuhakikisha ubadilishaji hati huo unakamilika, Lukuvi alisema Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, imehamisha wakurugenzi wanaohusika na masuala ya ardhi na kuimarisha Kanda ya Kati inayohudumia mikoa ya Dodoma, Singida na Morogoro ili kutoa huduma kikamilifu
0 maoni:
Post a Comment