Idadi ya vifo yaongezeka Sierra Leone

mediaKatika wilaya ya Regent, sehemu moja ya wilaya hiyo iliahtirika kwa maji, siku ya Jumatatu, Agosti 14. zaidi ya watu 300 walipoteza maisha.
Wakati ambapo zoezi la kutafuta miili mingine likiendelea katika wilaya yenye milima ya Regent katika mji mkuu wa Sierra Leone, Freetown, inaripotiwa kuwa idadi ya waathirika wa maporomoko ya udongo imeongezeka na kufika mia nne.
Maafisa wa usalama wamesema kwa zaidi ya miili mia moja imetolewa chini vifusi siku ya Jumanne na maiti zinaendelea kupatikana kutokana na zoezi gumu la uokozi linaloendelea.
Rais wa Sierra Leone, Ernest Bai Koroma, ameomba msaada wa dharura kwa nchi yake ili usaidie nchi hiyo kukabiliana na “uharibifu wa hali ya juu”.
Mazishi ya pamoja yamepangwa ili kupunguza msongamano wa maiti katika chumba cha kuhifadhia maiti.
Mpaka siku ya Jumatatu miili zaidi ya mia tatu ilikua imepatikana, kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Sierra Leone.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment