Soko la Sido Mkoani Mbeya limetetekea kwa moto usiku wa kuamkia leo na kutekteza mali mbalimbali ambazo thamani yake wala chanzo cha moto huo mpaka sasa hazijafahamika.
Akithibitisha kutokea kwa moto huo Mkuu wa Wilaya ya Mbeya William Ntinika amesema kuwa moto huo ambao uliwaka mpaka saa saba za usiku ulikuwa mkubwa na kuteketeza mali zote katika eneo la kuuzia vyakula.
Ntinika amesema kuwa jitihada mbalimbali zilifanyikaka katika kudhibiti moto huo bila kuzaa matunda ikiwani ni pamoja na kikokisi cha zima moto, Jkt, pamoja na magari ya zima moto ya kiwanda cha Songwe lakini moto ulikua mkubwa zaidi wakati ukiendelea kuwaka.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya William Ntinika.
Mkuu huyo wa Wilaya amesema kuwa anataraji kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa na pamoja na wilaya kukutana hii leo kwa ajili ya kufanya tathmini na kuunda tume itakaoyochunguza chanzo cha ajali hiyo.
0 maoni:
Post a Comment