Ukivalia viatu vyako bila soksi unajiweka katika hatari ya makubwa zaidi kuliko kunuka kwa miguu pekee.
Chuo cha tiba ya
miguu nchini Uingereza kinasema karibuni kumekuwa na ongezeko la
maambukizi ya maradhi yanayosababishwa na kuvu kutokana na kuvuma kwa
mtindo wa kuvalia viatu bila soksi, hasa miongoni mwa vijana.
Mtaalamu Emma
Stephenson anasema amekuwa akipokea wanaume wa kati ya miaka 18-25 walio
na matatizo kwenye miguu yao ambayo yametokana na kutovalia soksi au
kuvalia viatu visivyowatosha vyema.
Kutovalia soksi
siku hivi kumekuwa mtindo maarufu wa mavazi, na mwanamuziki Sam Smith ni
miongoni mwa watu wanaojitokeza hadharani wakiwa na viatu bila soksi.
Wanaume wengi katika maonesho ya mitindo pia mara nyingi huonesha mavazi wakiwa na viatu bila soksi.
Mwanamuziki
Tinie Tempah amejishindia tuzo nyingi kwa sababu ya mitindo na mara
nyingi katika maonesho ya mitindo ya Londo huketi viti vya mbele.
Yeye pia huwa mara nyingi havai soksi - lakini anafahamu madhara yake?
"Miguu ya binadamu kwa kawaida hutoa nusu painti (ambayo ni sawa na lita 0.28) ya jasho kila siku," Emma Stephenson anasema.
"Unyevu mwingi
na joto unaweza kusababisha maambukizi ya maradhi yanayotokana na kuvu
mfano ugonjwa unaosababisha mwasho na kuchubuka kwa ngozi (kwa
Kiingereza athlete's foot)."
Kwa mujibu wa Emma, madhara yake yanaweza kuwa mabaya.
"Moja ya visa
vibaya nilivyowahi kukumbana navyo ni cha mwanamume mmoja wa miaka 19
aliyefanya kazi ya kuosha magari. Miguu yake ilikuwa inatokwa na jasho
sana na ilikuwa imechubuka sana."
Lakini bila
shaka itachukua ujasiri kumwambia bingwa wa UFC Conor McGregor kwamba
anaweza kupata matatizo kutokana na mtindo wake wa kuvalia viatu.
Emma anashauri kwamba siri ni kutozidisha, iwapo bado utataka kutovalia soksi.
Jaribu usivae viatu bila soksi kwa muda mrefu.
Jaribu pia kuweka kitu cha kukausha jasho kwenye soli ya kiatu chako kabla ya kukivalia bila soksi.
Kadhalika, kuwa makini kuchunguza miguu yako. Ukigundua unaumwa pahali tafuta usaidizi upesi.
0 maoni:
Post a Comment