MSHIRIKA WA GAZETI LA GUARDIAN ASHIKILIWA.

Mshirika wa gazeti la Guardian, Ashikiliwa naSerikali ya uingereza ilimshikilia kwa muda mshilika wa mwandishi wa gazeti la Guardian katika uwanja wa ndege wa Heathrow chini ya sheria ya kupiga vita ugaidi.David Miranda mshirika wa mwandishi huyo wa habari aliyepokea taarifa za siri zilizo fichuliwa na mfanyakazi wa zamani wa shirika la upelelezi la taifa la Marekani,Edward Snowden,alishikiliwa zaidi ya masaa 9,hapo jana 18.8.2013 na kuzusha madai kwamba serikali inajalibu kuwatisha wale wanaoripoti juu ya suala hilo.Miranda,raia wa Brazil,alishikiliwa kwa muda ambao serikali inaruhusiwa kushikilia watu kwa ajili ya kuwasaili kwenye mipaka kwa kuzingatia sheria ya kupiga vita Ugaidi.Mirinda alikuwa anarudi nyumbani Brazil kutoka Ujerumani na simu yake.Kompyuta yake ya mkononi na vifaa vya kuhifadhi kumbukumbu kwenye koopyuta vimechukuliwa.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment