Wakati mashabiki wa kandanda kutoka sehemu mbalimbali wakiwasili Brazil kushuhudia fainali za kombe la dunia zinazoendselea nchini humo,nao raia wa nchi hiyo wanapanda ndege na kuondoka.
wanaenda kuishi katika nchi za jirani sababu ikiwa ni kupanda kwa gharama za maisha pamoja na makelele ya mashabiki wa soka ni ngumu kuamini kuwa kwa mashabiki wengi wa soka kuikimbia nchi yao kwa muda na kuwapisha na kuwapisha raia wanchi nyingine kuja kushuhudia michuano ya kandanda ya kombe la dunia inayo endelea nchini humo.
kwa mujibu wa shirika linalo usika na usafiri nchini Brazil,tokea mwaka huu uwanze asilimia 20 ya raia wamesafili kwenda nje ya nchi na kufanya kiwango hicho kuwa kikubwa ukilinganisha na kile cha mwaka jana cha mwezi juni na julai
lakini inadaiwa kuna baadhi ya raia wanakwenda kuishi nje ya nchi yao katika kipindi hiki cha fainali ya kombe la dunia ikiwa ni njia ya kujiongezea kipato zaidi kwa kukodisha makazi yao kwa mashabiki wa soka kutoka nje ya Brazil ambapo hadi sasa idadi yao imefikia laki tisa
mmoja kati ya nyota wa kandanda nchini Brazil na dunia nzima Ronaldinho Gaucho nae imembidi ahame katika nyumba yake hili akodishe katika michuano ya kombe la dunia kwa nia ya kujipatia kipato zaidi.Gaucho anaipangisha nyumba yake hiyo kwa dola 15,462 lakini imekuwa ikielezwa kuwa bei yake hiyo ni kubwa sana licha ya yeye mwenyewe kitetea kupitia katika mtandao wake wa Twitter.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 maoni:
Post a Comment