AJALI YAUA WATU 17 TANZANIA.

Watu 17 wamekufa na wengine kujeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea Mkoa wa Dodoma katikati mwa Tanzania.

Taarifa zinasema ajali hiyo imetokea baada ya magari mawili moja lori na jingine ni basi la abilia kugongana uso kwa uso.

Akizungumza na JICHOPEMBUZI kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma David misime amesema ajali hiyo ilitokea majira ya saa mbili za asubuhi  siku ya jumatano imesababishwa na kile ambacho kinasemekana ni uzembe wa dereva 

Hii sio mara ya kwanza kutokea ajari hapa tanzania ambapo sababu kadhaa zimekuwa zikitajwa kusababisha ajali  ikiwemo mwendo kasi wa magari,uzembe wa madereva pamoja na ubovu wa barabara.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment