IDADI YA VIFO VIMEONGEZEKA LIBYA.

Saa 24 za ghasia huko Libya zimesababisha vifo vya watu 61 na kuifanya idadi ya waliofariki kufikia takribani 150 katika wiki mbili za mapigano nchini humo

Takribani watu 38 waliuawa katika mji wa mashariki wa Benghazi wakati majeshi ya Libya yalipo pambana na wanamgambo wa kiislamu wenye silaha Jumamosi na Jumapili.

Wafanyakazi wa misri walikuwa miongoni mwa watu 23 waliouawa katika makao makuu ya Libya  Tripoli,ambapo mapigano makali kati ya makundi ya wanamgambo yanayopigana yameingia wiki ya tatu.

Karibu watu 100 wamefariki Dunia katika mapigano yanayo endelea katika uwanja wa ndege pekee tangu mwezi julai wakati majeshi ya serikali yakipata taabu kuzuia ongezeko la ghasia hizo tangu vita vya 2011.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment