Marekani imefunga ubalozi wake Libya kwa muda na wafanyakazi wake wote wameamishiwa nchi jirani Tunisia.
walipelekwa huko kwa magari huku wakilindwa na ndege za marekani.
Wizara ya mashauri ya nchi za nje ya Marekani pia imewasii raia wote wa Marekani waondoke nchini humo
Jengo la ubalozi wa Marekani mjini Tripoli lipo katika eneo ambalo limeathirika na mapambano kati ya makundi ya wapiganaji yanayo zozana ambayo yamekua yakigombaniana kudhibiti uwanja wa ndege wa kimataifa wa Libya.
Waziri wa mashauri wa nchi za nje John Kerry alisema kuwa kulikuwa na hatari hasa ikiwakabili wafanyakazi wa ubalozi huo,lakini alisisitiza kuwa shughuli za ubalozi zinasimamishwa kwa muda
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 maoni:
Post a Comment