Zinaitwa Afracan Music magazine Awards ambapo za mwaka huu zimetolewa huko Eisemann center Texas Marekani na kuhudhuriwa na mastaa mbalimbali akiwamo Diamond wa Tanzania ambaye pia alikuwa mmoja wa wanao wania tuzo
Good News za ushindi wote huu ni kwa mujibu wa meneja babu tale ambaye naye kaudhuria tuzo hizi Marekani aliye nitumia msg kwa kusema wametanga mkumbini kwamba Diamond ameshinda tuzo mbili moja ya msanii Bora wa Afrika mashariki na nyingine ni wimbo bora wa kushirikiana ambao ni "Number one Rmx "alioufanya na Divado wa Nigeria .
Kolabo bora ni single iliyokuwa inawaniwa na T PAIN na 2 Face -Rain Bow Khona ya uhuru na mafikizolo wa South Afrika Surulere Rmx ya Dr sid wa Nigeria Mkenya Amani Ft.Waganda Radio na Weasel "kiboko changu"
Tuzo ya msanii Bora afrika mashariki aliyo shinda Diamond ilikuwa inawaniwa pia na Ben Pol kutoka Tanzania ,Bebe cool wa Uganda,Wyre wa Kenya ,Navio wa Uganda ,na Jackie Gosee wa Ethiopia
Lady Jydee ameshinda tuzo ya msanii bora wa kike Afrika mashariki aliyekuwa anashindana na Rema wa Uganda.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 maoni:
Post a Comment