Uchunguzi wa JICHOPEMBUZI umebaini kuwa watu wa familia saba wameuawa katika mpaka baina ya Israel na Palestina uliozingirwa.
Barabara zinaonekana kuwa tupu na moshi mweusi unaonekana kutoka katika eneo la Gaza huku mitambo ya umeme ikiwa imezimwa baada ya matanki ya mafuta kupigwa .
![]() |
| mmoja wa waliopoteza ndugu katika shambulio la gaza |
Wanajeshi 10 wa Israel wameuawa siku ya jumatatu wakiwemo wapiganaji watano wa Hamas walioingia Israel kupitia maandaki ya chini kwa chini
Israel inasema imegundua mahandaki Ishirini na mbili ya chini kwa chini eneo la mpakani kuingia Israel yanayo unganisha mtandao mpana wa maandaki hayo.
maafisa wa Afya katika utawala wa palestina wanasema kuwa watu 60 wameuawa Israel inasema imeshambulia maeneo sitini yakiwemo makao yasio na mtu ya kiongozi wa kundi la Hamas Ismael Haniya na vituo vya Redio na runinga vya Hamas
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema kuwa nchi yake ni lazima ijiandae na operasheni ya muda mrefu katika ukanda wa Gaza.


0 maoni:
Post a Comment