WANAUME 4 waliokuwa wameshitakiwa kwa kosa la jaribio la kumuua aliye kuwa Jasusi wa Rwanda Generali Faustini kayumba Nyamwasa nchini Afrika kusini wamepatikana na kosa la hatia hilo.
Nyamwasa alipigwa risasi na kujeruhiwa mwezi juni mwaka 2010 nje ya nyumba yake mjini Johannesburg
Washukiwa wengine wawili akiwemo aliye kuwa Dereva wake nyamwasa walifutiwa mashitaka yao na hakimu Stanley mkhazi aliyetoa uhamuzi wa kesi hiyo.
Nyamwasa alikimbilia nchini Afrika kusini miezi kaadhaa baada ya kukosana na aliyekuwa mshirika wake Rais Paul Kagame
Sady Abdou,Hemed Dinengo Sefu,Amani Uriwani,Richard Bachisa ,Hassann Nduli,na Paskol Kanyandekwe,ndio wanaume sita waliokuwa wameshitakiwa kwa kupanga njama ya kumuua nyamwasa .wote walikanusha madai hayo.
Serikali imekanusha madai ya kuusika na jaribio la kumuua nyamwasa.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 maoni:
Post a Comment