Wananchi wa jiji la mbeya na vitongoji vyake vya jirani wanao itumia barabara kuu ya kutaka kuingia mjini hapa kupitia mji mdogo wa uyole eneo la makasini wamekupwa na adha kubwa ya Usafiri baada ya madereva wa malori kuegesha barabarani magari yao na kuifunga barabara hiyo.
Chanzo cha tukio hilo linalokwamisha shughuli za watu na kukwamisha uchumi kwa siku imepelekea Askari wa barabarani kukamata malori yaliyo paki pembezoni mwa barabara kung'oa namba za usajili wa malori hayo kutoza faini na kisha kutoa stakabazi bandia.
Madereva wa malori na matingokwa nyakati tofauti wameliambia JICHOPEMBUZI kitendo wanachofanyiwa si cha kistarabu na ni kinyume cha kazi yao kwa kuwa wamekuwa na mazoea ya kutoza toza kwa kinyume na utaratibu wa kutoa stakabadhi bandia
Mpaka timu ya JICHOPEMBUZI inang'atuka katika eneo hilo la tukio tayari msururu wa magari ulikwisha kuwa mrefu sana kwani magari yenyewe ni mengi yanayo toka nchi za jirani takribani 5 Drc Kongo,Zambia,msumbiji,south Afrika ,botuswana nk
wanachokitaka hasa wao ni kukutana na mkuu wa mkoa wa mbeya,Abbas Kandoro,na mbunge wa Mbeya mjini mh,Joseph Mbilinyi ambao awambo mkoani mbeya.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 maoni:
Post a Comment