madereva bodaboda wa mjini Iringa wakiingia uwanjani |
wakionesha shamrashamra katika sherehe hizo |
Mwigulu Nchemba akimuongoza Kamanda wa UVCCM Mkoa wa Iringa, Salim Asas kuwapongeza bodaboda hao |
Nchemba akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodaboda Mjini Iringa, Mwmbope Joseph |
MWENYE macho aaambiwi tazama; hivi ndivyo
unavyoweza kuzizungumzia sherehe za kumuapisha Kamanda wa Umoja wa
Vijana wa
Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa, Salim Abri maafuru kwa jina la
Salim
Asas.
Wale vijana machachari wa barabarani,
ambao hivi karibuni walijinasibu mbele ya kadamnasi kwamba wao ni CCM
damu jana
katika sherehe hizo wamedhihirisha tena kauli waliyoitoa kwenye kikao
chao na
uongozi wa SUMATRA kilichofanyika hivikaribuni kwamba wao ni CCM.
Vijana hao si wengine zaidi ya wale
wanaojulikana saaaana kwa kupamba misafara ya viongozi wa kisiasa. Ni
vijana
wanaogombaniwa na vyama vyote vya kisiasa, ni vijana wanaelezwa kuwa
mtaji
mzuri wa kisiasa pamoja na kwamba hawatabiriki, hao si wengine ni
madereva wa
vyombo vya usafirishaji vya miguu miwili na mitatu (bodaboda na bajaj).
Jana walikuwepo kwa mamia. Walizunguka mji
mzima wa Iringa wakiwa na bodaboda na bajaj zao, wakiwa wamevaa sare ya
kijani
ambayo ni vazi rasmi la CCM.
Msafara wao mrefu ulivutia wananchi wa
mjini hapa, wakajitokeza kwa wingi barabarani kuona msururu wao na jinsi
walivyokuwa wakiendesha vyombo vyao kwa mbwembwe.
Wakasaidia kuwavuta watu waliokuwa hawajui
au waliojifanya wameziba masikio kwamba hawajasikia Asas, kipenzi cha
wakazi wa
Iringa, anaapishwa kwa awamu ya tatu kuwa kamanda wa UVCCM.
Wakiwa na Kamanda Mteule, Asas na mgeni
rasmi wa sherehe hizo, Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba
walishiriki
uzinduzi wa matawi mapya ya CCM zaidi ya matano mjini hapa.
Na baadaye wakaongoza msafara wa viongozi
hao kuelekea uwanja wa Mwembetogwa ambako sherehe za kumuapisha Asas
zilikuwa
zikifanyika.
Pamoja na Bodaboda palikuwa na burudani
nyingine tosha, iliyopamba sherehe hiyo ambayo Asas mwenyewe aliita ni
sherehe
ya aina yake ambayo haijawahi kutokea katika historia yake ya kisiasa.
Ilikuwepo bendi ya muziki wa dansi ya
Vijana Jazz na wasanii wengine akiwemo Dokii na kundi lake, Makomandoo,
Baba
Level, Wanne Star na wasanii kibao wa mjini Iringa.
Mbali na wasanii hao kuwa gumzo kwa
burudani waliyotoa katika sherehe hizo, bodaboda walinogesha zaidi gumzo
hilo.
BONGO LEAKS ikapita vijiweni na kusikia
wale wapenzi wa kile chama kingine kilichotoa mbunge katika Uchaguzi
Mkuu wa
2010 wakisema kwa hasira.
“Wametukimbia, wametukimbia kwasababu ya
ubishi wa ndugu yetu Msigwa, Mchungaji Peter Msigwa anataka kutupa kazi
ngumu
ya kusaka kura 2015,” alisema mmoja wa vijana wa kijiwe cha stendi kuu.
Kijana huyu hajasikika, akapaza sauti
yake, ili Mchungaji Msigwa aisikie akisema……TUMEKWISHA.
Bodaboda wana matatizo makubwa pamoja na
kwamba ni mtaji mkubwa wa kisiasa. CCM inawasaidia, iko jirani nao kwa
raha na
shida lakini sisi tunasubiri tuwaite kwenye mikutano, tena kwa kuwapa
elfu tano
tano. Wapi na wapi? ASIYESIKIKA huyo alisema.
ASIYESIKIKA mwingine akasema walileta
matatizo yao kwetu Chadema na CCM. Wenzetu CCM wakawa wajanja,
wamewatekelezea
japo siyo yote lakini inawapa matumaini kwamba wamesikilizwa.
Ndio wenzetu CCM nasikia waliwapa mafunzo
ya udereva ili wajue sheria za barabarani. Zaidi ya madereva 800
wamefundishwa
bila kuchangia hata senti tano, wakatafutiwa ofisi, wakaanzisha chama
chao,
wakapema mtaji wa zaidi ya Sh Milioni tano kwa ajili ya kuanzisha Saccos
yao na
wakapewa pikipiki nne kwa ajili ya kukopeshana kwa mzunguko.
Sisi tumebaki na maneno, kila kukicha ni
kulalama tuuu Peoples Power…. People Power… halafu tuko mbali na
maendeleo ya
watu, nani atatuthamini? Tuoneshe basi kwamba tunajali matatizo ya watu,
tujitokeze kuwasaidia sio tu kwa kusubiri fedha za serikali na kwa
kutumia
fedha zetu maana hakuna serikali inayoweza kutatua matatizo ya watu wake
wote,
hiyo ni ndoto hata kwa mataifa tajiri.
ASIYESIKIKA mwingine akasema wanachofanyiwa
na CCM kinaongeza gharama; hatutawapata kirahisi tena katika misafara ya
viongozi wetu……watata ujira uongezeke, nani atatoa…… hilo linabaki
swalia kwa
wengi wetu
0 maoni:
Post a Comment