Sehemu ya CD Feki zilizokamatwa.
Msama akionesha CD zilizokamatwa katika maeneo ya Kariakoo na Kimara Bonyokwa.
Baadhi ya vifaa vinavyotumika katika kutengeneza CD feki zikiwa Kituo cha Polisi Urafiki.
Hizi ni sehemu ya CD feki zilizokamatwa.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akionyesha mashine ya kisasa
aina ya LG iliyokamatwa kutoka kwa watuhumiwa wa kurudufu kazi za
wasanii (CD FEKI) katika maeneo ya Kariakoo na Kimarta Bonyokwa jijini
Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande)
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama
akionesha mashine ya kisasa aina ya LG waliyokamatwa nayo watuhumiwa
wa kurudufu CD feki za kazi za wasanii katika maeneo ya Kariakoo na Kimara
Bonyokwa jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mrakibu Msaidizi wa Polisi ASP, Denis
Moyo. (Picha na Francis Dande)
Msama akionyesha wino na vifaa vingine vinavyotumika katika kutengeneza CD feki za kazi za wasanii.
Msama akionesha mashine ya kuprint Cover za CD.
CD feki zilizokamatwa katika maeneo ya Kariakoo.
Msama akizungumza na waandishi wa habari leo.
Lundo la CD feki zilizokamatwa katika maeneo ya Kimara na Kariakoo.
Kasha la CD iliyokuwa na nyimbo za mwimbaji Bahati Bukuku ikiwa imewekea stika feki ya TRA.
Baadhi ya CD feki zilizokamatwa na Kampuni ya Msama Auoctions Mart.
NA FRANCIS
DANDE
OPERESHENI
ya kukamata watuhumiwa wa wizi wa kazi za wasanii, imeshika kasi baada ya
Kampuni ya Msama Auction Mart kukamata mashine za kisasa za kurudufu kazi za
wasanii na CD feki zenye thamani ya shs. milioni 200.
Huo ni
mkakati wa kampuni hiyo kwa kushirikiana na Wizara ya Habari Vijana Utamaduni
na Michezo pamoja na Jeshi la Polisi katika vita ya kuwapigania wasanii waweze
kunufaika na kazi zao.
Mbali ya
wasanii, pia harakati hizo zinalenga kuiwezesha serikali kupata mapato yake
kutoka kwa wasanii ambao siku zote wamebaki duni huku wajanja wachache wakivuna
mamilioni ya fedha.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini
Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama
alisema operesheni hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki katika maeneo ya Kariaakoo
na Kimara Bonyokwa jijini Dar es Salaam.
“ Ttumekamata vijana watano ambao wapo katika
kituo cha Polisi cha Urafiki na
taratibu za kuwafikisha mahakamani zinafanyika,” alisema Msama.
Aidha, Msama amesema katika zoezi
hilo wanamshikiria mmiliki wa nyumba moja ambayo baadhi ya watuhumiwa walikutwa
wakifanya uharamia wa kudurufu kazi za wasanii, hivyo kuikosesha serikali
mapato yake halali.
“Kwa namna hii, serikali haiewezi
kupata mapato na pia wasanii wataendelea kuwa ombaomba kutokana na kuibiwa kazi
zao,” alisema Msama.
Msama alisema, zoezi hilo ni endelevu
na litafanyika nchi nzima ambapo kampuni Msama kwa kushirikiana na Polisi wa Kituo cha Urafiki, wameweza
kuwakamata jumla ya watuhumiwa 20 ambao wanasubiri taratibu za kisheria ili
kesi zao ziweze kufikishwa mahakamani.
Msama
aliongeza, matunda ya operesheni hiyo, yameanza kuonekana kwani kwa
kushirikiana na raia wema, wameweza kukamata mashine moja kubwa ya kisasa aina
ya LG ambayo huweza kuzalisha CD feki zaidi ya ishirini kwa dakika tano.
“Katika
kipindi kicha wiki moja tumekamata mzigo mkubwa wa shs mil.200 katika maeneo ya
Kimara Bonyokwa na Kariakoo na kazi bado inaenedelea,” alisma Msama.
Msama
aliyechangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya muziki wa injili nchini, amejitwika
jukumu hilo zito katika kupigania maslahi ya wahusika ambao wameshindwa kupiga
hatua kutokana na wiki wa kazi zao.
0 maoni:
Post a Comment