Jumatano
ya wiki iliyopita ndio liliibwa hili gari aina ya BMW lisilopenya
risasi ambalo huwa linakuwepo kwenye msafara wa Rais Kenyatta, na
taarifa ya Ikulu ilisema liliibwa wakati dereva wake ambae ni askari
alikua akielekea kwenye makazi ya Polisi Nairobi, njiani akasimamishwa
na watu waliokuwa na AK 47 wakamtupa mtaroni baada ya kumvua nguo na
kukimbia nalo.
Taarifa
mpya ambayo inaripotiwa na Julius Kepkoich toka Kenya inasema gari
hili limepatikana kwenye mji wa Tororo Uganda na tayari limepelekwa
Kampala baada ya msako uliofanywa na Polisi na kumkamata mshukiwa mmoja
hotelini mjini Bungoma.
Kikosi
cha Polisi wa Flying squard kikishirikiana na Interpol walivuka boda
na kuingia mji wa Tororo Uganda walikohisi kwamba ndiko kulikopelekwa
gari hilo.
Polisi
wanamshikilia Nelson Topicho aliyekamatwa Bungoma na anatarajiwa
kurejeshwa Nairobi ili kuhojiwa zaidi ambapo kikosi kingine cha Nakuru
Kenya kinamshikilia Agrey Odhiambo anaetuhumiwa kukarabati gari
lililoibwa na kumiliki bunduki huku Nairobi wakitarajiwa kumuhoji upya
dereva wa Ikulu David Muchui.
0 maoni:
Post a Comment