![]() |
Kamishna KOVA akiwa katika mkutano huo |
Kamishna
wa Polisi Kanda Maalum Dar es salaam Suleiman Kova amewataka askari
wote wa Kanda hiyo kufanyakazi kwa weledi, kuzingatia haki za
binadamu, na kufuata maadili ya kazi katika utendaji wao wa kila siku.
Kamishna
Kova ameyasema hayo wakati akiongea na Maafisa na Wakaguzi katika kikao
cha utendaji kilichofanyika katika ukumbi wa Bwalo la Maafisa
Oysterbay, Kinondoni, jijini Dar es Salaam na kusisitiza umuhimu
wakutoa huduma bora kwa wateja kulingana na matarajio ya wananchi.
Aidha Kamishna
Kova amesisitiza usiri katika Taarifa zinazoletwa /zinazotolewa na
wananchi na kwamba kwa kufanya hivyo kutalifanya Jeshi la Polisi
kuaminika kwa wananchi. Akizungumzia suara la rushwa, Kamishina Kova
amewaasa askari kutojihusiasha na kupokea rushwa kwani ni adui wa haki
na kinyume na maadili ya kazi za Polisi.
Amehimiza
ushirikishwaji wa wananchi katika kila hatua hasa katika mashauri
mbalimbali ya kesi zao na kutenda kazi kwa uwazi hasa wakati wananchi
wanapotakiwa kupata taarifa za mashauri yao au wanapoomba ushauri katika
kero zinazowasibu.
0 maoni:
Post a Comment