Katibu Mkuu wa NATO Anders Fogh Rasmussen
Viongozi wa nchi za Magharibi
wameishutumu Urusi kwa "ushawishi" wake katika mgogoro wa Ukraine,
mwanzoni mwa mkutano wa viongozi wa Nato huko Wales, Uingereza.
Nato na Uingereza zimeonya kuwa shinikizo juu ya
Urusi litaongezeka iwapo haitabadili msimamo wake kuhusu eneo la
mashariki mwa Ukraine.
Kikao cha viongozi wa Nato, Wales, Uingereza
Nchi za magharibi zinasema zina ushahidi kwamba Bwana Putin anawaunga mkono wapianzani wanaotaka kujitenga kutoka Ukraine kwa kuwapa mafunzo ya kijeshi na silaha, lakini Urusi inakana tuhuma hizo.
Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa zaidi ya watu milioni moja wamelazimika kuyakimbia makaazi yao mashariki mwa Ukraine.
Mkuatano huo wa siku mbili mjini Newport utatawaliwa na mjadala kuhusu mgogoro wa Ukraine.
0 maoni:
Post a Comment