MBUNGE WA JIMBO LA KALENGA AWAONYA WAPIGAKURA WAKE KUTOSHIRIKI MAANDAMANO YASIO NA TIJA , ATAKA WASHIRIKI KULETA MAENDELEO



Mbunge  wa  jimbo la  kalenga Bw. Godfrey  Mgimwa  akitoa  salam  zake kwa  waumini wa kanisaa la romani cathoric parokia ya  Ifunda  leo .
Mbunge wa jimbo la Kalenga  Godfrey Mgimwa akipongezwa na mwenyekiti wa kwaya ya Mtakatifu Secilia parokia ya Ifunda bAmadea Mwehange mara baada ya  kukabidhiwa msaada wa Tsh milioni 2 kwa ajili ya  kuingia studio kurekodi 
Paroko wa kanisa la RC Ifunda  Alois Mdemu wa  tatu kulia akiwa na  wahisani mbali mbali wanaosaidia kanisa  hilo kutoka  nchini Ujerumani pamoja na mbunge wa  jimbo la Kalenga Godfrey Mgimwa wa nne  kulia 
Paroko Mdemu  akimweleza jambo mbunge Mgimwa kabla ya  kuwashukuru  wahisani hao kutoka Ujerumani 
Mbunge Mgimwa akiwashukuru  wahisani  toka Ujerumani ambao  wanasaidia misaada mbali mbali kanisani hapo
Mbunge Mgimwa  kulia akipewa maelekezo baada ya kutembelea  chuo cha ufundi cha kanisa  hilo 
Mgimwa akitazama kivaa cha kubebea  vinywaji  kilichotengenezwa kwa mbao 
Waumini wa kanisa  hilo  wakifuatilia salam za mbunge wao 

Paroko  wa kanisa  la RC Ifunda Alois Mdemu  akimpongeza mbunge Mgimwa kwa mchangowake katika  jimbo la Kalenga 

..........................................
Na  matukiodaima.co.tz 

WAKATI viongozi wa umoja  wa katiba  ya  wananchi (UKAWA)wakitishia  kufanya maandamano yasio ya  kikomo kushirikiza bunge la katiba  kushitishwa ,mbunge wa jimbo la kalenga Godfrey Mgimwa amewataka wanakalenga kutoshiriki maandamano yasio ya kimaendeleo Kwao.

Mbali ya kuwataka kuepuka maandamano hayo pia amewataka waumini wa dini mbalimbali Kalenga kufanya Kazi ya kuombea amani ya nchi ili bunge hilo limalizike salama na kupata katiba bora itakayolivusha Taifa miaka 50 zaidi.


Akitoa Salam zake wakati akikabidhi msaada wa Tsh milioni 2 kwa wanakwaya wa mtakatifu secilia parokia ya Ifunda na matenki mawili ya maji katika zahanati ya kanisa hilo jana ,mbunge Mgimwa alisema kuwa mbali ya kulipongeza kanisa hilo kwa kuendelea kuombea amani bado alisema Kazi kubwa ni kuendelea kuombea bunge la katiba na amani ya nchi.


Kwani alisema bunge hilo la katiba linalokaribia kufika mwisho mwezi ujao ili liweze kumalizika kwa heri na mafanikio ni vema watanzania wote kuelekeza Sara na dua zao kuwaombea wajumbe wa bunge la katiba ili waweze kumalizia mchakato huo salama.


" waumini wenzangu na wapiga kura wa jimbo langu la kalenga mimi mbunge wenu nawawakilisha vema katika kuwaletea maendeleo ......hivyo nawaombeni tushirikiane kufanya maandamano ya kuliletea jimbo letu maendeleo sio maandamano ya kuvuruga amani yetu"


Alisema ni vema wanakalenga kuwakwepa wale wote wanaopandikiza chuki dhidi ya watanzania na wale wanaoanzisha maandamano yasio na tija.


Kuhusu utekelezaji wa ahadi zake jimboni mbunge huyo alisema hadi sasa ana kila sababu ya kujivunia maendeleo makubwa ambayo amepata kuyaleta jimboni.


Kwani alisema hadi sasa jimbo la kalenga ni jimbo pekee katika Mkoa wa Iringa ambalo ameweza kuwaunganisha wapiga kura wake na vicoba na hadi sasa ahadi mbali mbali amepata kuzitekeleza ndani ya miezi mitatu japo ubunge wake ni wa mwaka mmoja pekee.


Hata hivyo alisema kuwa kwa wananchi wa Kalenga kwa sasa ndoto zao kuwa na maendeleo na hivyo iwapo wananchi wake watajiepusha na maandamano yasiyo kwisha ni vema kujielekeza nguvu zao katika ndoto ya maandamano ya kufanya Kazi kwa juhudi zaidi ili jimbo hilo liweze kupiga hatua zaidi katika maendeleo.


Kwa upande wake Paroko wa kanisa hilo Alois Mdemu pamoja na kushukuru kwa jitihada za mbunge huyo bado alisema jimbo la kalenga limepata mbunge wa kweli kutokana na matendo yake.


Alisema baada ya kifo cha mbunge wao mwaka huu Dr Wiliam Mgimwa wananchi wa jimbo hilo walianza kujihisi wapweke na kuvunjia moyo kuwa hawatapata mbunge mwingine kama aliyetangulia ila imekuwa tofauti baada ya mbunge wao huyo kufanikiwa kufanya makubwa zaidi.


Hivyo alisema wajibu wake kanisa kiongozi wa kanisa ni kuzidi kumuombea mbunge Godfrey Mgimwa ili azidi kuwatumikia wana kalenga na Taifa.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment