![]() |
Patrick Ole Sosopi . |
Matokeo
ya uchaguzi mkuu wa baraza la Vijana wa chama cha Demokrasia na
maendeleo ( Chadema) yametangazwa huku mwanasiasa Mkazi wa Mkoa wa
Iringa akipenya nafasi ya umakamu Mwenyekiti bara.
Katika
uchaguzi huo wa BAVICHA uliofanyika jana jijini Dar es Salaam, nafasi
ya Mwenyekiti ilikwenda kwa Patrobasi Katambi na Zeudi Abdalla
alichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti Zanzibar.
Kuchaguliwa
kwa Sosopi kushika nafasi hiyo nyeti ndani ya chama hicho kumeelezwa na
baadhi ya wafuatiliaji wa siasa za mkoa wa Iringa kwamba kunamuongezea
nguvu kisiasa.
Patrick Ole Sosopi ambaye ni baba wa mke mmoja na mwenye mtoto mmoja, ni mmasai aliyezaliwa na kukulia mkoa Iringa.
Ana
umri wa miaka 28. Ni msomi wa shahada ya kwanza ya Biashara na Utawala
(rasilimali watu) kutoka chuo kikuu cha Ruaha (RUCO). Kwa sasa kazi zake
ni kufuga ng'ombe.
Historia
yake ya uongozi ilianzia akiwa shule ya msingi, sekondari hadi chuo
kikuu cha RUCO ambapo alikuwa waziri wa Fedha kwenye serikali ya
wanafunzi 2011/2012.
Alijiunga
rasmi na CHADEMA mwaka 2009 alipokuwa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza
akiamini ni chama pekee ambacho kina tija ya kuboresha maisha ya jamii
yake ya kimasai na changamoto mbalimbali ambazo zilikuwa zikiwakabili.
Aliaminiwa
na vijana wa Ismani na kupata kura zote bila kupingwa na kuwa
Mwenyekiti wa BAVICHA jimbo la Ismani. Baada ya kushauriwa na
kushauriana na familia yake na vijana mbalimbali kutoka sehemu
mbalimbali za Tanzania, aligombea nafasi ya Umakamu Mwenyekiti wa
BAVICHA Bara na ameshinda.
Ingawa
ni mojawapo wa wasomi wachache kwenye jamii yao ya kimasai, ni mtu
ambaye usomi wake haujamfanya asahau mila na tamaduni za kimasai.
Chakula chake, mavazi yake, desturi yake ya maisha ya kila siku ni
desturi za kwao na zenye kuhuwisha Utanzania.
0 maoni:
Post a Comment