Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amezindua mradi wa upanuzi wa kituo cha umeme ambacho ni cha pili kwa ukubwa ncini humo,mradi unao fadhiliwa na china na kuendeshwa na kampuni ya ujenzi ya china
Upanuzi wa kituo cha Umeme cha kusini cha kariba utaongeza uwezo wa zimbabwe kuzalisha umeme kwa robo baada ya miaka mitatu ijayo,mradi huo utagharimu dola za kimarekani milioni 533 ambapo dola milioni 319 zitapatikana kupitia mkopo utakao tolewa na benki ya Exim ya China.
Hata hivyo,kuzinduliwa kwa mradi huo kumekuja baada ya ziara ya Rais Mugabe kwenda china kuanzia Agosti 24 hadi 28 wakati huo alisaini mikataba mingi ya makubaliano ikiwemo msaada wa serikali wa dola milioni 20 za kimarekani na mkopo wa dola milioni 218 kwa kampuni ya mawasiliano ya Net One ya zimbabwe .
Home / Uncategories / RAIS WA ZIMBABWE AZINDUA MRADI WA UPANUZI WA KITUO CHA UMEME ULIOFADHILIWA NA CHINA.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 maoni:
Post a Comment