Uingereza haina budi kushiriki katika hujuma dhidi ya IS

 Kwa mujibu wa waziri wa mambo ya nchi za nje Philip Hammond,Uingereza haina njia nyengine isipokuwa kujiunga na hujuma za madege ya nchi shirika dhidi ya wanamgambo wa kigaidi wa dola la kiislam-IS.Kwakua wanamgambo hao ni kitisho kwa nchi yake na kwa utulivu wa eneo lote la Mashariki ya kati,"watu hawana budi",anasema waziri huyo wa mambo ya nchi za nje wa Uingereza.Bunge la Uingereza linatarajiwa hii leo kupiga kura kama nchi hiyo ishiriki katika hujuma za kijeshi za nchi shirika nchini Irak.Inatarajiwa wengi wa wabunge wataunga mkono mpango huo.Hammond ameondowa lakini uwezekano kwa nchi yake kujiunga na hujuma hizo dhidi ya wanamgambo wa itikadi kali wa dola la kiislam -IS nchini Syria.Idadi ya raia wa Umoja wa Ulaya wanaopigana upande wa magaidi wa kiislam nchini Iraq na Syria inakisiwa imeongezeka na kufikia watu 3000.Mapema mwaka huu idadi yao ilikadiriwa kufikia waatu 2000.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment