WHO inategemea tiba kwa kutumia damu

Shirika la afya la Umoja wa mataifa WHO linauwekea matumaini makubwa uwezekano wa kuwatibu wagonjwa wa Ebola kwa damu ya wale waliopona maradhi hayo.Watu wanajiwekea matumaini makubwa upande huo-shirika la WHO linasema.Tiba hiyo inatuwama katika matumaini kwamba katika damu ya manusura kuna viini maalum vinavyoweza kuwasaidia wagonjwa.Madaktari wawili wa kimarekani walioambukizwa virusi vya Ebola nchini Liberia walitibiwa kwa damu ya wagonjwa waliopona.Wote wawili ni wazima hivi sasa.Shirika la afya la Umoja wa mataifa WHO halikubainisha lakini kama hali hiyo imesababishwa na matibabu hayo ya aina yake au huduma bora za afya nchini Marekani.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment