Urusi yawapagia marufuku baadhi ya viongozi wa Umoja wa Ulaya kuingia nchini humo

 Katika ugonvi kati ya Umoja wa Ulaya na Urusi,serikali mjini Moscow inasemekana imeandaa orodha ya majina ya wanasiasa wa Umoja wa Ulaya ambao hawataruhusiwa kuingia nchini humo.Hayo amearifiwa na ubalozi wa Ujerumani mjini Moscow,amesema mwenyekiti wa kundi la wabunge wa chama cha walinzi wa mazingira katika bunge la Ulaya,Rebecca Harms mjini Brussels.Mwanasiasa huyo wa chama cha walinzi wa mazingira cha Ujerumani alikuwa katika uwanja wa ndege wa Moscow jana na kukataliwa ruhusa ya kuingia nchini humo.Alikuwa aende Moscow kusikiliza kesi dhidi ya rubani mmoja wa helikopta wa Ukraine.Sababu mojawapo aliyopewa ya kukataliwa kuingia Urusi ni kwamba ameunga mkono vikwazo vya Umoja wa Ulaya dhidi ya Urusi, anasema mwanasiasa huyo.Uamuzi wa Urusi wa kumkatalia ruhusa mbunge Rebecca Harms umewakasirisha wengi miongoni mwa wakuu wa Umoja wa Ulaya.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment