Kundi la Dola la Kiislamu limekamata maeneo mapya kutoka
kwa majeshi ya Syria mashariki mwa mji wa Deir al-Zor leo,
ikiwa ni mafanikio yake ya kwanza katika eneo hilo katika muda
wa miezi miwili. Wapiganaji kutoka kila upande wameuwawa
katika mapambano hayo mjini Deir al-Zor, mji ulioko kilometa
450 kaskazini mashariki mwa Damascus katika jimbo
linalopakana na Iraq. Dola la Kiislamu , ambalo linalengwa katika
mashambulio ya anga ya Marekani nchini Iraq na Syria ,
limekamata maeneo makubwa ya eneo la viwanda la Deir al-Zor,
ikiwa na maana kuwa kundi hilo sasa linadhibiti zaidi ya nusu
ya mji huo. Mkuu wa shirika linaloangalia haki za binadamu
nchini Syria Rami Abdul Rahman amesema kundi hilo la
wanamgambo wa Kiislamu , ambalo linapambana na majeshi ya
Wakurdi kuudhibiti mji wa Kobani katika mpaka na Uturuki
limepeka wapiganaji zaidi mjini Deir al-Zor katika siku za karibuni.
Wakati huo huo Uingereza imesema leo imeidhinisha kupelekwa
ndege zenye silaha na zisizo na silaha zinazoruka bila rubani
kwa ajili ya uchunguzi wa kijasusi katika anga ya Syria, ili
kupata taarifa za kijasusi za kundi la Dola la Kiislamu
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 maoni:
Post a Comment