Watu 21 wauwawa Baghdad


Mabomu  mawili  yaliyotegwa  katika  gari  katika  eneo  la  Washia kaskazini  mashariki  mwa  Baghdad leo, yamesababisha  vifo  vya kiasi  ya  watu 21. Miripuko  hiyo  katika  eneo  la  kuegesha  magari katika  eneo  la  Talbiyah, ambayo  pia  imewajeruhi  kiasi  watu  40, ilikuwa  ya  hivi  karibuni  kabisa  katika  wimbi  la  mashambulizi  ya mabomu  yanayolenga  jamii  ya  Washia  walio  wengi  katika  mji mkuu  ambayo  imesababisha  watu  40  kuuwawa  katika  muda  wa siku  tatu. Hakuna  kundi  lililodai  mara  moja  kuhusika  na mashambulio  hayo  ya  mabomu, lakini  kundi  la  jihadi  la  Dola  la Kiislamu, ambalo  limekamata  maeneo  makubwa  ya  Iraq  tangu mwezi  Juni , limesema  limefanya  mashambulio  mengine  kama hayo  katika  siku  za  hivi  karibuni. Majeshi  ya  Usalama  na wanamgambo  wa  Kishia  wamewazuwia  wapiganaji  wa  Dola  la Kiislamu  kuingia  katika  mji  huo  mkuu baada  ya   miezi  kadhaa ya  mapigano  makali, lakini wanamgambo  hao  bado  wanauwezo wa  kufanya  mashambulio  ya  mabomu  kila  siku  mjini  Baghdad.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment