Kuporomoka kwa hadhi ya mwanariadha nyota anayekimbia kwa
miguu ya bandia Oscar Pistorius kutoka mwanariadha nyota wa
kimataifa kumekamilika leo wakati alipopelekwa katika jela mjini
Pretoria kuanza kutumikia hukumu ya miaka mitano jela.
Pistorius atakuwa mmoja kati ya wafungwa 7,000 katika gereza
la Kgosi Mampuru , ambako alipelekwa saa chache baada ya
kuhukumiwa kwa kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp katika
siku ya wapendao mwaka jana. Likijulikana hapo zamani kama
gereza la kati mjini Pretoria , jela hiyo inafahamika kwa ukatili
dhidi ya wafungwa wa kisiasa walioshikiliwa chini ya utawala
wa kibaguzi ambao ulianguka miaka 20 iliyopita.
Wakati huo huo Waafrika kusini wameeleza kukatishwa kwao
tamaa na hukumu ya miaka 5 aliyopewa Pistorius , wengi
wakisema amepata hukumu nyepesi kwa kumuua mpenzi wake
Reeva Steenkamp. Wizara ya sheria imesema kimsingi
mwanariadha huyo atatumikia miezi 10 tu jela.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 maoni:
Post a Comment