Upinzani nchini Tanzania umetia saini makubaliano ya pamoja ,kuking'oa madarakani chama tawala.
Utiaji huo saini makubaliano ya kukishinda chama tawala cha mapinduzi CCM katika uchaguzi ujao umefanywa na viongozi wa vyama vinne huku tukio hilo likishuhudiwa na wafuasi wao.
Katibu mkuu wa chama cha upinzani CHADEMA ,Dr.Willbrod slaa ni mwingoni mwa viongozi walio tia saini makubaliano hayo na amesema vyama ivyo vitasimamisha wagombea wake kwa pamoja kwenye ngazi zote za uchaguzi kuanzia serikali za mitaa mpaka ngazi ya Urais .
Katibu mkuu wa chama cha wananchi CUF Maalim seif Sharif Hamad amesema tukio hilo la vyama kusaini makubaliano ya kufanya kazi kwa pamoja kwa lengo la kuing'oa CCM ni muhimu na la kihistoria.
Viongozi walio tia saini walaka huo wa makubaliano ni Freeman mbowe mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani CHADEMA ,Profesa Lipumba mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF katibu mkuu wa chama hicho ambaye pia ni makamu wa kwanza wa Zanzibar Maalim seif sharif Hamad ,James mbatia mwenyekiti wa NCCR mageuzi ,Mosena nyambabe katibu mkuu wa NCCR mageuzi Dr.Emmanuely makaidi mwenyekiti wa NLD
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 maoni:
Post a Comment