Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini
Watu watatu
wa familia moja wamefariki dunia baada ya kukatwa mapanga, huku mmoja
wao akitenganishwa kichwa na kiwiliwili kwa madai ya ugomvi wa urithi wa
mali.
Kamanda wa Polisi Mkoa Kagera, Henry Mwaibambe, alisema waliokufa papo hapo ni baba wa familia, Sadick Khamis (84), aliyekatwa kichwa na kutenganishwa na kiwiliwili pamoja na mkewe Zamda Sadick (44).
Mwingine ni mtoto wa wanafamilia hao, Juma Sadick (15), ambaye alifariki wakati akipatiwa matibabu katika hospitali teule ya wilaya ya Rubya.
Kamanda Mwaibambe alisema wauaji hao waliivamia familia hiyo saa 2:45 usiku wa juzi na kuwatendea unyama ambao chanzo kikisadikiwa kuwa ni urithi hasa kutokana na kuwapo kwa ugomvi wa muda mrefu katika familia hiyo.
“Marehemu alioa wake wanne huku Zamda akiwa mke mdogo. Ulikuwapo ugomvi katika familia kwa madai baba wa familia alikuwa na mapenzi na mke huyo mdogo hali iliyopelekea mauaji hayo ya kinyama,” alisema Mwaibambe.
Alisema wakati wa tukio hilo, mtoto mwingine wa kike wa baba huyo, Aza Sadick (19), hakudhuriwa na badala yake wauaji hao walichukua simu yake ya mkononi.
Kufuatia kadhia hiyo, mtoto mkubwa wa baba huyo, Issa Sadick (49), anashikiliwa na polisi akidaiwa kuhusika na mauaji hayo kutokana na kuwa na mgogoro mkubwa na baba yake.
Kwa mujibu wa kamanda huyo, uchunguzi zaidi kuhusiana na tukio hilo unaendelea.

0 maoni:
Post a Comment