KONGAMANO LA TAASISI YA MWALIMU NYERERE KUHUSU MCHAKATO WA KATIBA LAINGIA DOSARI


Waliokuwa wasemaji wakuu katika kongamano hilo ni pamoja na wajumbe wa iliyokuwa tume ya mabadiliko ya Katiba akiwemo aliyekuwa mwenyekiti wake Jaji Mstaafu Joseph Warioba.

Kongamano hilo lililofanyika jijini Dar es Salaam lilivunjika baada ya baadhi ya vijana kufanya vurugu wakati Jaji Warioba akitoa ufafanuzi wa Ibara mbalimbali za katiba Pendekezwa.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku alieleza masikitiko yake makubwa baada ya vijana hao kufanya vurugu hizo.


Hata hivyo akasema hawatakatishwa tamaa na vurugu hizo na badala yake watajipanga kikamilifu ili waendelee na midahalo hiyo kwa njia ya amani. 

Taarifa kamili kuhusiana na kongamano hilo utaletewa kesho................................
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment