Rais Wa TAFF Simon Mwakifamba akiongea wakati wa uzinduzi wa Tuzo za Filamu Nchini zilizozinduliwa hivi karibuni.
Mkurugenzi wa Bodi ya FIlamu Nchini Mama Fisoo akiongea wakati wa Uzinduzi wa Tuzo za Filamu nchini
Novemba 24, 2014; Zile tuzo zilizosubiriwa kwa muda mrefu na
watanzania sasa zimezinduliwa rasmi jijini Dara es Salaam. Zimezinduliwa
rasmi kwa shamra shamra za aina yake mwishoni mwa wiki na Naibu katibu
mkuu wa Wizara ya Habari, vijana, utamaduni na michezo Prof. Elisante
Ole Gabriel, kwa niaba ya Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo. Uzinduzi huo uliohudhuriwa na wadau, wasanii na wageni
mbalimbali wanaounga mkono tasnia hiyo hapa nchini, ni ishara rasmi
kuwa pazia la tuzo hizo zinazotarajiwa kufanyika mwakani sasa liko wazi.
Tuzo hizo ambazo hazijawahi kutokea nchini zimeandaliwa na
Kampuni ya Binary And Pixel LTD kwa kushirikiana na Shirikisho la Filamu
Tanzania.
Tuzo hizo zitakazoshindaniwa katika vipengelezaidi ya Thelathini (30), hii ni nafasi nzuri na yakipekee kwa wana tasnia ya filamu nchini na kuonesha ukomavu na kukubalika kwa tasnia hiyo nchini. Tuzo hizo zinatarajiwa kufanyika mapema 2015 jijini Dar es Salaam na zitakuwa zikifanyika kila mwaka.

Akiongea katika uzinduzi huo kwa niaba ya Waziri wa Habari,
vijana, utamaduni na michezo, Naibu katibu mkuu wa wizara hiyo Prof.
Elisante Ole Gabriel alisema kuwa tasnia ya filamu imepiga hatua kubwa
nchini na hata nje ya nchi kwani kazi inaonekana. “Kwanza kabisa
niwapongeze Shirikisho la Filamu Tanzania kwa kuandaa tuzo hizi
zitakazoleta ufanisi katika tasnia ya filamu nchini.
Nina Imani kuwa mmejipanga kukabiliana na changamoto katika soko la kimataifa, hii ni kuwa tayari na kujiandaa kukamilifu kukabiana nazo kwa kuwa na kazi zenye ubora mkubwa, kutambulika kimataifa kwa uzuri wa kazi mnazozifanya, kutangaza nchi yetu kimataifa kupitia filamu na hata kuongeza pato la taifa kwa kazi zenu.”

Naye Raisi wa Shirikisho la Filamu Tanzania Simon Mwakifwamba
alisema kuwa wanayofuraha kubwa kama shirikisho kuandaa tuzo hizo kwani
inaonesha kukua kwa soko la filamu nchini kwa kasi na hata kuleta tija
katika jamii.
“Tunawashukuru wote mliofika kutuunga mkono katika ufunguzi rasmi wa tuzo hizi za Filamu nchini, kwa namna ya pekee tunawashukuru wadhamini wetu Sadolin Paints, Appex, na Hak neel, tunaomba wadau wengi zaidi wajitokeze kudhamini tuzo hizi kwani ni kuonesha uzalendo kwa kupenda na kuthamini vya nyumbani. Kwa kufanya hivyo tutakua tumeunga mkono jitihada kubwa zinazofanywa na wadau wa tasnia hii ya filamu nchini,” alisema Mwakifwamba.

Hii ni fursa pekee kwa wadau wa Tasnia ya filamu nchini kukuza
na kutangaza kazi zao katika soko la kimataifa hivyo hawana budi
kuichangamkia fursa hii kwa kupeleka kazi zao walizozifanya na kujaza
fomu ili kuingia katika kinyang’anyiro cha tuzo hizo kubwa nchini katika
tasnia hiyo.
Fomu zinapatikana katika ofisi za Shirikisho la Filamu Tanzania zilizopo mtaa wa Ikungi-Kinondoni B jijini Dar es Salaam au waweza pata katika mtandao kwa kutembelea www.taff.or.tz. Mwisho wa kujiandikisha ushiriki na kuwasilisha kazi katika kuwania tuzo hizo ni 15/12/2014.

0 maoni:
Post a Comment